Fair Work Commission ni mahakama ya kitaifa ya mahusiano ya mahali pa kazi ya Australia. Inasaidia wafanyakazi na waajiri kutatua masuala kazini.
Masuala ya kawaida ni pamoja na kufukuzwa kazi bila haki, uonevu, unyanyasaji wa kingono, ubaguzi, na migogoro kuhusu haki za mahali pa kazi.
-
Fair Work Commission inaweza kukusaidiaje?
Nchini Australia kuna sheria zinazotumika kazini bila kujali umetoka wapi, hali yako ya visa, au ni muda gani umekaa Australia.
Nyenzo:
-
Karatasi ya ukweli: Nini maana ya Fair Work Commission? (pdf)
-
Kigae cha Mitandao ya Kijamii: Fair Work Commission inaweza kukusaidia kutatua matatizo kazini (jpg)
Ili kupata usaidizi katika lugha yako, tumia Translating and Interpreting Service kwa kupiga simu 131 450. Mwambie opereta lugha yako, sema unapiga simu kuhusu Fair Work Commission, na umpe nambari ya simu 1300 799 675.